Bei
Tiketi za kulipia bila ada ya InvitePro
Tiketi za kulipia hazina ada ya InvitePro. SMS na WhatsApp hulipiwa kwa kifurushi: SMS 300, WhatsApp 500, SMS + WhatsApp 700 kwa mhudhuriaji. Barua pepe ni bure. Wanunuzi wanakulipa wewe moja kwa moja.
SMS
TZS 300
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
TZS 500
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
SMS + WhatsApp
TZS 700
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
Ada kwa kila tiketi ya kulipia
Bure
- Tiketi za bure (kuingia bila kulipa): hakuna ada.
- Tiketi za heshima (complimentary) unazotoa wewe: hakuna ada.
- SMS na WhatsApp kwa wanunuzi na wahudhuriaji zinalipiwa kwa kifurushi cha jumbe; barua pepe ni bure.
Maswali
Maswali kuhusu bei
Pesa za tiketi zinaenda wapi?
Moja kwa moja kwako. Mnunuzi analipa namba yako ya M-Pesa, Lipa namba au akaunti ya benki kwa maelekezo unayoweka. InvitePro haishiki pesa za tiketi zako.
Mnunuzi anapataje tiketi yake?
Baada ya kulipa, mnunuzi anaweka namba ya muamala. Wewe au mhudumu wako anathibitisha, na tiketi yenye QR inatumwa kwa SMS, WhatsApp au email. Hahitaji kupakua programu yoyote.
Kuna ada ya kila mwezi?
Hakuna ada ya mwezi. Tiketi zinatolewa bila ada kwa kawaida; ada yoyote ya tiketi ikiwapo inaonyeshwa kwenye bei. SMS na WhatsApp hutumia kifurushi kwa kila mhudhuriaji, na barua pepe ni bure.
Tunakaguaje tiketi mlangoni?
Wahudumu wanafungua skana kwa PIN na kuskani QR. Mtandaoni, mfumo huzuia tiketi iliyopokelewa kutumika tena. Skana zikiwa bila mtandao, kila simu hufanya kazi na orodha yake; wahudumu waratibu ili QR ileile isipokelewe kwenye milango miwili.
Naweza kuuza tiketi kwenye tovuti yangu?
Ndiyo. Weka kitufe cha "Nunua tiketi" kwenye tovuti yako kwa mstari mmoja wa msimbo, au shiriki kiungo cha ukurasa wa mauzo kwenye WhatsApp na mitandao ya kijamii.