Uza tiketi mtandaoni. Rahisisha mapokezi mlangoni. Fuatilia mauzo, pokea malipo moja kwa moja na skani tiketi kwa QR mlangoni.
Inavyofanya kazi
Kutoka tukio hadi mlangoni kwa hatua nne
- 1
Tengeneza tukio
Weka tarehe, ukumbi na aina za tiketi: VIP, Kawaida, Early bird — kila moja na bei na idadi yake.
- 2
Shiriki kiungo
Tuma kiungo cha mauzo kwenye WhatsApp, Instagram au tovuti yako. Mawakala wako wanapata viungo vyao.
- 3
Pokea malipo
Mnunuzi analipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki — moja kwa moja kwako — kisha unathibitisha.
- 4
Kagua mlangoni
Tiketi zenye QR zinaskaniwa kwa simu yoyote. Unaona walioingia kila dakika.
Huduma
Kila kitu cha kuuza tiketi
Kwa waandaaji wa gala, makongamano, matamasha, semina na michezo.
Aina za tiketi
VIP, Kawaida, Meza ya watu 10, Early bird. Weka idadi, tarehe za mauzo na aina zilizofichwa kwa msimbo maalum.
Malipo kwa simu
Maelekezo yako ya malipo (M-Pesa, Lipa namba, benki) yanaonyeshwa kwa mnunuzi. Anaripoti muamala, wewe unathibitisha.
Tiketi zenye QR
Kila mhudhuriaji anapata tiketi yake yenye jina na QR kwa SMS, WhatsApp au email — pamoja na kikumbusho kabla ya tukio.
Ukaguzi mlangoni
Viungo vya skana vyenye PIN na ruhusa kwa aina za tiketi. Mapokezi ya bila mtandao husawazishwa baadaye; wahudumu huratibu skana ili QR ileile isipokelewe mara mbili.
Mawakala wa mauzo
Kila wakala ana kiungo chake. Unaona mauzo yao na kamisheni wanayostahili, na unarekodi malipo yao.
Misimbo ya punguzo
Punguzo la asilimia au kiasi, kwa aina fulani za tiketi, na kikomo cha matumizi.
Bajeti ya tukio
Panga matumizi, rekodi gharama na wauzaji, na linganisha na mapato ya tiketi.
Kitufe kwenye tovuti yako
Kitufe cha "Nunua tiketi" kinachofungua ukurasa wa mauzo ndani ya tovuti yako.
Bei
Tiketi za kulipia bila ada ya InvitePro
Tiketi za kulipia hazina ada ya InvitePro. SMS na WhatsApp hulipiwa kwa kifurushi: SMS 300, WhatsApp 500, SMS + WhatsApp 700 kwa mhudhuriaji. Barua pepe ni bure.
SMS
TZS 300
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
TZS 500
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
SMS + WhatsApp
TZS 700
kwa mhudhuriaji, kwa tukio
Ada kwa kila tiketi ya kulipia
Bure
- Tiketi za bure (kuingia bila kulipa): hakuna ada.
- Tiketi za heshima (complimentary) unazotoa wewe: hakuna ada.
- SMS na WhatsApp kwa wanunuzi na wahudhuriaji zinalipiwa kwa kifurushi cha jumbe; barua pepe ni bure.
Maswali
Maswali yanayoulizwa mara nyingi
Pesa za tiketi zinaenda wapi?
Moja kwa moja kwako. Mnunuzi analipa namba yako ya M-Pesa, Lipa namba au akaunti ya benki kwa maelekezo unayoweka. InvitePro haishiki pesa za tiketi zako.
Mnunuzi anapataje tiketi yake?
Baada ya kulipa, mnunuzi anaweka namba ya muamala. Wewe au mhudumu wako anathibitisha, na tiketi yenye QR inatumwa kwa SMS, WhatsApp au email. Hahitaji kupakua programu yoyote.
Kuna ada ya kila mwezi?
Hakuna ada ya mwezi. Tiketi zinatolewa bila ada kwa kawaida; ada yoyote ya tiketi ikiwapo inaonyeshwa kwenye bei. SMS na WhatsApp hutumia kifurushi kwa kila mhudhuriaji, na barua pepe ni bure.
Tunakaguaje tiketi mlangoni?
Wahudumu wanafungua skana kwa PIN na kuskani QR. Mtandaoni, mfumo huzuia tiketi iliyopokelewa kutumika tena. Skana zikiwa bila mtandao, kila simu hufanya kazi na orodha yake; wahudumu waratibu ili QR ileile isipokelewe kwenye milango miwili.
Naweza kuuza tiketi kwenye tovuti yangu?
Ndiyo. Weka kitufe cha "Nunua tiketi" kwenye tovuti yako kwa mstari mmoja wa msimbo, au shiriki kiungo cha ukurasa wa mauzo kwenye WhatsApp na mitandao ya kijamii.
Tukio lako lijalo, tiketi zake mtandaoni
Fungua akaunti kwa dakika mbili na uanze kuuza leo.
Anza kuuza tiketi